Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru leo Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.
Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.
Hati ya Mashitaka ya Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya Mashitaka matatu lakini Julai 22 mwaka 2015, Hakimu Mkazi Mary Moyo alitoa uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu katika mashitaka mawili yaliyosalia ambalo ni kosa la pili na la tatu .
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ilimfungia dhamana Sheikh Ponda baada ya kukubaliana na hati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), wakati huo Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam liloomba Mahakama hiyo imfungie dhamana mshitakiwa huyo chini ya Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai ya Mwaka 2002.
Hatua hiyo ya kufunguliwa kesi katika Mkoa wa Morogoro ilikuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Agosti 19 Mwaka 2013 saa Tatu asubuhi, kumfutia kesi ya jinai Na.144/2013 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano baada ya DPP kudai kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki katika kesi hiyo No.144/2013 kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Hata hivyo baada ya hakimu Liwa kumwachilia huru,Ponda ambaye aliletwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na wanausalama wa polisi na magereza chini ya ulinzi mkali, alikamatwa tena na kupakizwa kwenye magari ya wanausalama hao ambapo baadhi ya wanausalama hao waliliambia gazeti hili kuwa wanampeleka Ponda mkoani Morogoro kwaajili ya kufunguliwa makosa matatu ya uchochezi, kufanya mkusanyiko haramu na kisha akarejeshwa gereza la Segerea Dar es Salaam , lakini baadae Uongozi wa Jeshi la Magereza uliamua kumuamisha Ponda kutoka Gereza la Segerea na kumuamishia Katika Gereza Moja Mkoani Morogoro.
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, baada ya kuwasili kwa helikopta ya Jeshi la Polisi katika uwanja wa gofu mjini Morogoro.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate, Mwanasheria Kiongozi wa Serikali, Bernard Kongola, alidai kuwa Agosti 10, mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
Alidai kuwa Sheikh Ponda ambaye anatetewa na wakili wa kujitegemea Juma Nassor aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.
Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa Mei 9, mwaka 2010, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.
Katika shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.
Kwamba, Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa huko ni Wakristu.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Filed Under:
MATUKIO
on Monday, November 30, 2015
Post a Comment