Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
WAKATI Rais John Pombe Magufuli akitegemewa kutangaza Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa, matumbo ya wabunge yamepata moto wakijiuliza kama watawezana na kasi yake endapo watateuliwa kuwemo.
Magufuli, ambaye Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimuita Tingatinga, ameweka wazi katika hotuba yake kwa Bunge kuwa hatamvumilia mtu mzembe na mvivu na kwamba watakaobainika kujihusisha na rushwa au ufisadi, watashughulikiwa.
Ingawa wabunge karibu wote walikuwa wakimshangilia kwa nguvu wakati wa hotuba yake hiyo, inadaiwa hamu ya kupata ulaji wa uwaziri inawafanya baadhi yao kuingiwa na woga, kwani ufanyaji kazi wa mazoea ndiyo unaowatesa.
“Nakuambia hapa wabunge, hasa wale wenye ndoto za kuteuliwa uwaziri wana wasiwasi kama wataweza kweli kwenda na kasi ya huyu jamaa, maana anaonekana kuwa siriaz sana na kazi.
Hili liko wazi maana wengi walizoea kuona nafasi za juu kiuongozi wanazitumia kwa masilahi yao,” kilisema chanzo chetu katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Inadaiwa wengi wa wanaotegemea kupata uwaziri wana hofu kwa sababu wanaamini mzigo watakaopewa utakuwa mkubwa kuliko tabia na hulka zao.
Rais Magufuli ameahidi kuteua Baraza dogo la Mawaziri litakalokuwa limesheheni wachapakazi na katika kukabiliana na vitendo vya rushwa na ufisadi, alisema kazi hiyo ataifanya kwa dhati.
Hata hivyo, mbali na jina la Tingatinga hivi sasa mtaani amepewa jina jipya la Mtumbua majipu licha ya kuwa kitendo hicho huleta maumivu.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Post a Comment