Mara nyingi familia au ndoa nyingi zinapokumbwa na tatizo la kukosa watoto lawama nyingi huelekezwa zaidi kwa wanawake jambo ambalo si sahihi sana kwani kuna wakati tatizo hilo huweza kuchangiwa na kinababa pia.
Ni vyema ikafahamika kwamba wanaume nao huweza kuwa sababu ya matatizo ya uzazi kwa na uchunguzi hulazimika kufanyika kwa kuangalia mbegu za uzazi na kupima korodani.
Mwanaume unaweza kujifahamu kama unatatizo endapo utakuwa na dalili zifuatazo, licha ya kwamba siyo lazima zote zijitokeze lakini mojawapo ni upungufu wa nguvu za kiume.
Moja ya dalili kubwa ni kuishi na mwanamke zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mimba, hii huashiria uwepo wa tatizo hapo.
Pia tatizo hili huweza kuambatana na dalili za mwanaume kutoa manii nyepesi sana na zenye harufu mbaya, manii nyepesi hutoka mara moja ukeni unapomaliza tu tendo la ndoa.
Aidha, mwanaume huweza kuzongwa na maumivu ya muda mrefu ya korodani, maumivu ya kiuno, maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara, uvutaji wa sigara kwa muda mrefu, unywaji wa pombe kali, na matumizi ya madawa ya kulevya mfano bangi na mirungi na mengineyo yanayofanana na hayo.
Mambo yanayohitajika kufanyika
Matatizo haya huweza kutambulika kupitia kwa daktari wa matatizo ya uzazi kwenye hospitali za mikoa. Vipimo vya mbegu za uzazi vitafanyika kuangalia kiwango cha mbegu na ubora wake kama zina uwezo wa kutungisha mimba.
Vipimo vingine itategemea na uwepo wa matatizo mengine ya uzazi kwa mwanaume kama kuwahi kumaliza tendo la ndoa, kushindwa kufanya tendo la ndoa, upungufu wa nguvu za kiume, uchovu mkali baada ya tendo la ndoa, maumivu ya kiuno, korodani na maumivu ya njia ya mkojo.
Post a Comment