Ili kupata maendeleo sehemu yeyote ile nilazima kuwa na vitu muhimu kama barabara, umeme, hospital, Shule pamoja na maji.
Daraja likiwa limebomolewa na kusombwa na maji tangu mvua zilizonyesha mwaka jana. Picha hii inaonesha ubovu wa miundombinu ya barabara inayotoka Vikindu
kuelekea Kazole Magenge 20 kupitia kijiji cha Cheta kwenda hadi Magodani
mkoa wa Pwani.
Sisi tukiwa kama
wananchi na wakazi wa Cheta, Kazole pamoja na Magodani, tunaomba
serikali mtusaidie kutengeneza barabara hii ili tuweze kusafirisha
bidhaa zetu kwa usalama zaidi pamoja na kupata punguzo la nauli maana
hadi sasa nauli kutoka Vikindu hadi Magodani ni Tsh 1,500/= kwa mtu
mmoja, na kwa kipindi cha mvua nauli upanda hadi 2,500/= iyo ni kwa
gari.
Kwa makadrio umbali wa kutoka Vikindu hadi Magodani ni kama 14KM hivi, kwaiyo tunaomba mtusaidie sana kwa jambo hili maana tunateseka sana.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Kwa makadrio umbali wa kutoka Vikindu hadi Magodani ni kama 14KM hivi, kwaiyo tunaomba mtusaidie sana kwa jambo hili maana tunateseka sana.
Post a Comment