Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

RISASI ZALINDIMA KASKAZINI MWA PARIS

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Ufyatulianaji mkali wa risasi umetokea kaskazini mwa Paris katika mtaa wa Saint Denis na ripoti zinasema operesheni ya polisi kuhusiana na mashambulio ya Ijumaa inaendelea.

Maafisa kadha wa polisi wamejruhiwa, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.

Shirika la habari la AFP lanasema Abaaoud Abdelhamid, anayedaiwa kupanga mashambulio hayo, ndiye aliyekuwa akisakwa kwenye operesheni hiyo mtaa wa Saint Denis.

Afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa, mwandishi wa BBC James Longman
Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia wakisema milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri saa za Ufaransa.

Naibu meya Stephane Peu amewahimiza raia wasalie manyumbani, akisema "hili si shambulio jipya bali ni operesheni ya polisi".

Polisi wamewaondoa raia kutoka eneo hilo. Awali, duru za kiusalama zilisema video ya kiusalama ilikuwa imeonyesha huenda kulikuwa na mshambuliaji wa tisa mashambulio hayo ya Ijumaa.

Watu 129 walifariki kwenye mashambulio yaliyotokea maeneo sita mjini Paris.

Kundi la Islamic State (IS) limesema ndilo lililotekeleza mashambulio hayo.

Ripoti moja inasema barabara zimefungwa eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis.

Uwanja wa taifa wa michezo wa Stade de France, ambako washambuliaji walilipua mabomu Ijumaa, umo kwenye mtaa huo.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top