Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGEA NA WAFANYAKAZI

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.

Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam.

Jana ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

"Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.

Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.

Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, NOVEMBA 23, 2015.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top