SIRI nje! Sakata la mmiliki wa Kliniki ya Tiba Asilia ya Fore Plan iliyopo Ilala Bungoni, Dar, Dk. Juma Mwaka ‘JJ Mwaka’ kufanyiwa ziara ya kushtukiza na baadaye kudaiwa kumkimbia Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla limechukua sura mpya huku mambo mengi yaliyomponza yakifichuka.
Risasi Jumamosi limechimba.
SOO LILIVYOKUWA
Siku chache baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri, Dk. Kigwangalla alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho kinachosifika kwa kutoa tiba ya asili badala ya hospitali (tiba mbadala), hasa kwa wanawake wanaosumbuliwa na matatizo ya uzazi.
Katika hali ya kushangaza, matatibu na manesi waliokuwa kazini walitokomea kusikojulikana na kuwatelekeza wagonjwa, wakikwepa kuonana na waziri huyo ambaye akiwa na msafara wake.Walifanya ukaguzi wa kina kwenye kituo hicho. Kufuatia kitendo cha Dk. Mwaka na wenzake kuingia mitini.
Waziri Kigwangalla alitoa amri ya kufungwa kwa muda kwa kituo hicho mpaka uchunguzi wa kina utakapokamilika ili kuona kama huduma zinazotolewa zinakidhi vigezo na ni salama kwa wagonjwa.
MITANDAO YAMCHOMA
Simulizi ya jinsi tabibu huyo alivyosimamishwa kutoa huduma ili kupisha uchunguzi na ukaguzi wa kina, inaanzia mbali ambapo kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya kuaminika, chokochoko kuhusu huduma zake zilianzia kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa kipindi kirefu kulikuwa na makundi mawili yanayoshindana kwenye mitandao ya kijamii.
Kundi la kwanza ni wale waliowahi kutibiwa katika kliniki hiyo na kufanikiwa kupona matatizo yao. “Hawa walikuwa wakimtetea kwamba anatoa huduma sahihi lakini kundi jingine ni wale waliotibiwa na kupoteza fedha nyingi bila kupona matatizo yaliyokuwa yakiwasumbua.
“Hawa ndiyo waliochangia kwa kiasi kikubwa kuifumbua macho Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kwani walitaka dawa na huduma za Dk. Mwaka zichunguzwe kwa vile walishapoteza imani naye,” kilisema chanzo chetu makini kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
KUANIKA MAISHA YAKE MTANDAONI Kwa mujibu wa chanzo kingine, tabia ya Dk. Mwaka kupenda kuanika maisha yake kwenye mitandao ya kijamii ni suala jingine lililomponza na kufanya watu waanze kutilia shaka utajiri wake.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment