Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WANANCHI 2,857 WALIOKUMBWA NA MAFURIKO MOROGORO WAPOKEA MSAADA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Wananchi 2,857 waliopitiwa na mafuriko yaliyosababisha yumba zaidi ya 379 kubomoka na nyingine 997 kuingia maji katika kata ya magomeni wilaya ya kilosa mkoani Morogoro wameanza kupatiwa misaada ya chakula ingawa inahitajika misaada ya haraka ya dawa za binadamu, vyandarua pamoja na mahema ili kuwakinga na maradhi yanayoweza kujitokeza.

Wakizungumza wakati wa kupokea misaada hiyo waathirika wa mafuriko hayo wamewashukuru kampuni ya Alsaid pamoja na wabunge akiwemo mbunge wa viti maalumu mkoa wa Morogoro Devota Minja kwa jitihada zao walizo zionyesha toka kutokea kwa mafuriko hayo huku wakiomba serikali kuwasaidia kwa mambo mengine kama Mahema,vyandarua, pamoja na dawa kwa kujikinga na magonjwa ya milipuko.

Kwaupande wake mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya ALSAID Mbaraka Alsaed amesema kampuni yake itaendele kuwasaidia wahanga hao huku akiziomba taasisi mbalimbali na mashirika kuwasaidia wahanga hao ilinao waweze kuishi hasa katika kipindi hiki kigumu kwao.

Nao wabunge akiwemo mbunge wa jimbo la kilosa Mbaraka Bawaziri ameshukuru misaada mbalimbali inayo endelea kutolewa na wahisani huku mbunge viti maalumu mkoa wa morogoro devota minja akisema ipo haja ya serikali kuangalia swala la ujenzi wa tuta la mto mkondoa ili lisiendelee kesababisha hasara kwa watanzania na serikali.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top