Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Wanawake wa kijiji cha Messe wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wamelalamikia tatizo la ukosefu wa zahanati katika kijiji hicho hali ambayo inawalazimu wengi wao kujifungulia nyumbani kutokana na kushindwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya katika maeneo ya vijiji vya jirani.
Wanawake hao wanasema kwa muda mrefu wamekuwa wakitaabika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika maeneo ya vijiji jirani hali ambayo inachangia wanawake wengi kujifungulia kwenye mazingira ambayo siyo salama kufuatia tatizo hilo wameiomba serikali kuangalia uwezekno wa kuwajengea kituo cha kutolea huduma ya vipimo kwa ajili ya wanawake wajawazito na watoto ili kuwezesha wanawake waishio katika kijiji hicho kupata huduma bora za afya ya uzazi.
Mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya Siha Rashidi Kitambulio anakiri kijiji hicho kukabiliwa na tatizo la ukosefu wa zahanati ya kutolea huduma za afya na kwamba tayari halimashauri ya wilaya hiyo imetenga kiasi cha shilingin milioni 132 kwa ajili ya ujenzi ambao tayari umeanza.
Mapema akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa zahanati hiyo ambayo ujenzi wake umeanza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw.Amos Makalla ameauagiza uongozi wa halimashauri ya wilaya ya Siha kuhakikisha ujenzi wa zahanati hiyo unakamilika mapema ili kuwaondolea wananchi hususani wanawake wajawazito adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Post a Comment