Wazazi wawashauri watoto wao wafanye vibaya kwenye mitihani wilaya ya Songea.
Wakati serikali ikitangaza elimu bure kwa shule za msingi na sekondari bado katika kata za Lilai na Muhukuru ambazo ziko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wazazi katika kata hizo wamekuwa wakiwaambia watoto wao waandike majibu yasiyo sahihi kwenye mitihanii ili wafeli huku wakifanya sherehe mtoto anapofeli mtihani wa darasa la saba na pia hutorokea Msumbiji serikali inapowafuatilia.
Hayo yamesemwa na afisa tarafa wa tarafa ya Muhukuru iliyoko Songea mkoani Ruvuma Bi.Salma Mapunda wakati mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Benson Mpesya akizungumza na wananchi na walimu wa kata za Lilai na Muhukuru kuhusu sera ya serikali ya elimu bure.
Kutokana na hali hiyo mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Benson Mpesya ametangaza kuwachukulia hatu wazazi ambao watoto wao wamefaulu darasa la saba lakini hawajaripoti shule za sekondari ilhali serikali imeondoa gharama kwa shule za msingi na sekondari.
Kwa upande wao wazazizi wanaoishi kata za Muhukukuru na Lilai mpakani mwa Tanzania na msumbiji wamesema ni kweli tabia ya kufurahia mtoto anapofeli ipo lakini kwa sasa imepungua kutokana na sera ya serikali ya elimu bure kwa shule za msingi.
Post a Comment