Tatizo la kukatika umeme mara kwa mara linasababisha ukosefu wa mapato ya Serikali.
Uongozi wa kampuni ya ACACIA inayomiliki migodo ya dhahabu ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara imelalamikia changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara katika migodi yake huku wakilitaka shirika la ugavi wa umeme Tanesco kufanya jitihada za haraka kutatua tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu na kuikosesha kuikosesha serikali mapato yakutosha.
Akizungumzia hali hiyo kaimu meneja uzalishaji katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Bw.Salvatory Tesha amedai hali ya upungufu wa umeme na kukatika mara kwa mara imekua ikiisababishia kampuni ya ACACIA hasara huku mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Vitta Kawawa akiuhakikishai uongozi wa kampuni ya acacia kuwa tatizo hilo litakwisha siku za karibuni kwakuwa TANESCO inaendelea kujenga njia kubwa ya umeme kutoka singida kupitia mkoa wa shinyanga.
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Bw.Graham Crew amekabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni mia saba kumi na nne na laki nane fedha ambayo ni sehemu ya koidi ya matumizi ya ardhi kwa halmashauri ya msalala ambapo mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Vitta Kawawa amewataka viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo kusimamia na kuhakikisha fedha hizo zinatumika kujenga miradi ya maendeleo huku mkurugenzi wa halmashauri ya msalala bw.patrick kalangwa akidai baadhi ya fedha hizo zitatumika kutatua changamoto ya madawati katika shule za mzsngi na sekondari ili kutekeleza agizo la rais John Pombe Magufuli.
Post a Comment