Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Zaidi ya wanafunzi 100 waacha kwenda shule kutokana na mahudhurio duni ya walimu.
Wanafunzi zaidi ya 100 waliokuwa wakisoma shule ya msingi Buyuni iliyopo kata ya Mkalamo wilayani Korogwe wameacha shule kwa sababu mbali mbali ikiwemo mahudhurio duni ya walimu kwa sababu ya umbali wa makazi na eneo la shule pamoja na baadhi ya wazazi wa jamii ya wafugaji kushindwa kuwahimiza watoto wao kwenda shule.
ITV imeshuhudia shule hiyo ikiwa imebakiwa na madawati huku kukiwa hakuna mwanafunzi hata mmoja ambapo mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Buyuni Bwana.Mathayo Sungura amesema idadi kubwa ya wanafunzi wa shule hiyo ni jamii ya wafugaji ambapo mahudhurio yamekuwa yakishuka siku hadi siku kwa sababu ya changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa maji.
Baadhi ya wazazi wa jamii ya wafugaji walipoulizwa kuhusiana na changamoto ya watoto wao kushindwa kufika shuleni,wamesema wanafunzi wamekuwa watoro kwa sababu mahudhurio ya walimu shuleni hayaridhishi hatua ambayo imechangia baadhi ya wazazi jamii ya wafugaji kuwaruhusu watoto wao kwenda kuchunga.
Kufuatia hatua hiyo afisa elimu ya msingi bwana leyana alipotafutwa kwa njia ya simu kuelezea suala hilo amesema kuwa anafahamu changamoto hiyo lakini kwa hiv isasa amehamishiwa katika manispaa ya moshi hivyo atawasilianna wenzake waliopo wilayani korogwe ili aweze kupatikana msemaji wa elimu wilayani Korogwe.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Post a Comment