Kamati ya maafa nchini yatakiwa kuongeza misaada mkoani Tabora.
Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora imetoa rai kwa kamati ya maafa nchini kuongeza misaada mbalimbali ili kuwawezesha wananchi wahanga wa mvua wilayani humo wanaoendelea kukumbwa na changamoto ya nyumba zao kubomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw, Said Shabani Ntahondi wakati akikabidhi maturubai zaidi ya mianne ili kuwawezesha wahanga wanaoendelea kulala nje, ili wapate sehemu ya kujikimu, kwa kuwaondolea adha ya kunyeshewa mvua.
Aidha afiasa kilimo wilayani humo Bw, Absalom Kajuna amesema kuwa, poamoja na juhudi za halmashauri kupeleka misaada ya awali bado kuna changamoto kubwa ya kuwafikia wahanga kutokana na miundombinu kuharibika sana ambapo zaidi ya kata kumi zinaendelea kuathiriwa na mvua.
Post a Comment