Mvua zaharibu ekari zaidi ya 9,000,kaya 35 na mtu mmoja kufa kwa mafuriko Hanang.
Kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa zinazodhaniwa kuwa za El-Nino wilayani Hanang mkoani Manyara,zaidi ya ekari 9,000 za mazao ya Alizeti,Mahindi na Maharagwe zimeharibiwa kwa kufunikwa na maji,kuzolewa ama pia kushindwa kupaliliwa,huku pia mtu mmoja akifariki dunia na takribani kaya 35 za wananchi wa kijiji cha Mulbadaw zikiharibiwa na mafuriko,changamoto ambayo huenda mvua hizo zikaendelea kusababisha majanga makubwa kwa wakazi waishio mabondeni na mashamba sanjari na uhaba wa chakula.
Afisa kilimo,ushirika na umwagiliaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw.Paul Mollel ametoa angalizo hilo wakati kamati ya maafa ya wilaya hiyo ilipokutana kuwapa pole kwa kutoa msaada wa kilio 3,900 za nafaka ya mahindi kwa kaya 35 za kijiji hicho kukosa chakula na makazi baada ya mafuriko hayo kuharibu makazi na vifo vya mifugo mikubwa na midogo,mafuriko ambayo yanatishia pia ziwa bassotu kujaa na kutishia usalama wa wananchi waliopembezoni mwa ziwa hilo huku parokia ya kanisa katoliki ikibaki kisiwani.
Akikabidhi magunia 39 yanafaka ya mahindi kwa wakazi walioathiriwa zaidi katika kijiji cha Mulbadw,mwenyekiti wa kamati ya maafa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Hanang Bw.Thobias Mwilapwa amesema ingawa bado wilaya hiyo inahitaji msaada zaidi wa mahema na chakula hasa kutokana na madhara zaidi ya mvua amewataka wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni kuanza kuondoka.
Post a Comment