Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha lafanikiwa kupunguza ajali za barabarani.
Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabara mkoa wa Arusha limesema ushirikiano wa jeshi ilo na wadau wa usalama barabarani ikiwemo ITV na Radio One umefanikisha kupunguza ajali kwa kiasi kikubwa kutoka ajali miambili na arobaini mwaka 2014 hadi ajali hamsini na tano na vifo hamsini na tano hadi ishirini na moja hali inayoonesha mafaniko makubwa katika harakati hizo.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha jeshi la polisi mkoa wa Arusha Marison Mwakyoma ametoa kauli hiyo jijini Arusha alipokuwa anazungumza na Tazama Line na kusema kuwa mchango wa wadau wa usalama barabarani kuelimisha madereva na wananchi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa huku akivishukuru vyombo vya habari ikiwemo ITV na Radio One kwa mchango mkubwa kupitia vipindi vyake vya taarifa za usalama kwenye Radio One na vipindi vingine kwenye ITV.
Kwa upande wao madereva wakiwemo wanao endesha magari katika maeneo ya vijiji wamesema baada ya mafanikio makubwa katika maeneo ya mijini sasa nguvu zaidi ielekezwa vijijini huku wadau wa usalama barabarani wakieleza umuhimu wa serikali kushirikia nao na ikiwezekana kuwepo na fungu maalum kutoka serikalini la kusaidia juhudi hizo.
Post a Comment