Ukosefu wa madawati wasababisha wanafunzi kusomea nje wakiwa wamekaa chini.
Wanafunzi wa shule ya msingi Simanjiro kata ya Emboreti mkaoni Manyara wanalazimika kusomea nje wakiwa wamekaa chini kwenye vumbi,na wengine kubanana kwenye madawati chakavu kutokana na shule hiyo kukabiliwa na ukosefu wa madawati,na vyumba vya madarasa.
Mkuu wa shule hiyo mwalimu Lightness Lukumai amesema madawati yaliyopo shuleni hapo ni chakavu ambayo hayatoshelezi idadi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo hali ambayo inawafanya walimu wachache waliopo katika shule hiyo kufanyakazi katika mazingira magumu.
Amesema muamko wa wananchi wa jamii ya kimasai kusomesha watoto kwa sasa ni mkubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma na kwamba changamoto kubwa ni utoro unaosababishwa na wanafunzi kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa sita kufika shuleni.
Mratibu wa elimu shule za msingi kata ya Emboret Bw.Kastul Benedict amesema hali ya elimu katika kata hiyo siyo ya kuridhisha kutokana na wanafunzi kushindwa kufanya vizuri kitaaluma kutokana na uwepo wa changamoto za utoro,upungufu wa walimu pamoja na muamko mdogo wa wanachi wa jamii ya kimasai kusomesha watoto wa kike.
Baadhi ya wananchi wa jamii ya kimasai katika kata ya Emboret wanaiomba serikali kuboresha shule zilizopo katika maeneo ya wafugaji ili ziweze kutoa elimu bora kwa kuwa wananchi wa jamii hiyo wengi wao wamehamasisika kupelejka watoto wao shule.
Post a Comment