Shilole amesema hayo kupitia Account yake ya Instgram ambapo alikuwa akiwataka vijana wasikate tamaa na wala wasikubali kukatishwa tamaa na binadamu bali wanapswa kumtegemea Mungu na kusimamia kile ambacho wao wenyewe wanaamini kinaweza kusimamisha na kuja kubadili maisha yao.
"Nilipotoka ni mbali sana ni Mungu ndio anajua hivyo usikubali kukatishwa tamaa na binaadamu kaza ! Coz huwezi jua ridhiki yako ipo Wapi! some times huwa mnaona kama nawachekesha Ila mnapaswa mjifunze kupitia mimi haswa kinadada, mazuri yangu chukueni Mabaya yangu yaacheni! Jifunzeni kujituma na kutokata tamaaa mimi ningekata tamaaa nisingefika hapa nilipo na tumtangulize Mungu mbele" Alisema Shilole.
Shilole na kati ya wanamuziki wa kike ambao mwanzo walipoanza muziki watu walikuwa na mengi ya kusema juu yake huku wengine wakisema hawezi kuimba, wengine wakiponda kazi zake lakini baadae walielewa nini anakifanya kutokana na ukweli kwamba alipuuza maneno ya watu ambao walikuwa na lengo la kumkatisha tamaa, na sasa Shilole ni kati ya wasanii ambao wameweza kubadili maisha yao kupitia kazi ya muziki na anaendesha maisha kwa kazi hiyo.
Post a Comment