Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Wafanyabiashara wa machinjio ya nyama ya Babati watishia kugoma.
Wafanyabiashara wa machinjio ya nyamaya halmashauri ya mjini Babati mkoani Manyara wametishia kugoma kuchinja mifugo kuepuka kuvunja kanuni za afya endapo halmashauri ya mji huo haitakarabati barabara ya machinjio hayo kutokana na kuchoshwa kukodisha vijana kuwabebea nyama hizo vichwani umbali mrefu ili kuzipakia kwenye magari maalum ya usafirishaji kutokana na magari hayo kukwama kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha huku wakilalamikia kulipia ushuru unaokadiria kufika zaidi ya milioni 70 kwa mwaka.
Licha ya kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu ya wafanyabiashara hao kudai kutotatuliwa na halmashauri ya mji huo yakiwemo mazingira ya machinjio hayo kutokuwa ya kisasa, ITV iliweka mtego alfajiri na mapema na kushughudia wafanyabiashara hao wakiwa wameegesha vyombo vya usafirishaji wa nyama hizo umbali mrefu huku wakisomba shehena ya nyama ya Ng’ombe 50 wanaodaiwa kuchinjwa kila siku kwa siri hali ambayo hutishia usalama wa afya za walaji.
Nao baadhi ya wakazi wa mji wa Babati walioshuhudia ubebaji huo wa nyama wameeleza kutoridhishwa na hali hiyo huku wakiitaka halmashauri hiyo kusitisha biashara hiyo kwa muda kupisha ukarabati wa barabara hiyo ili kuepusha madhara ya afya kwa walaji na kuepusha milipuko ya magonjwa hasa wakirejea wa kipindupindu ulioanza januari 26 na kusababisha kulazwa kwa wagonjwa 47 katika hospitali ya Mrara ya halmashauri ya mji huo.
Nae kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji huo Bi Rena Urio ambaye pia ni mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi amekiri kutokea kwa hali hiyo huku akidai halmashauri inakabiliwa na miundo mbinu ya barabara kadha wa kadha za mji huo zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha na imeshafanya tathimi ya matengenezo ya barabara hiyo.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Filed Under:
BIASHARA
on Sunday, February 14, 2016
Post a Comment