Umeibuka mgogoro wa ardhi kati ya mwekezaji kampuni ya AVIV na wananchi wa kijiji cha Mihango wilayani Mbinga mkoani Ruvuma ambapo baada ya mwekezaji kutaka kuchukua ardhi ya wananchi wamewashambulia afisa tarafa ya kigonsera na mtendaji wa kata ya kigonsera na kuwafunga kamba na kisha kuwaweka kwenye mahabusu ya kijiji huku waking’oa alama zilizowekwa na mwekezaji mashambani.
Wakizungumza na Mutalemwa Blog kwenye mashamba yao katika kijiji cha Mihango wamesema kuwa wameamua kuwaadhibu afisa tarafa ya kigonsera Ebick Ilomo na afisa mtendaji wa kata ya Kigonsera Bw.Eliakim Mngongo kwa kuwapiga na kuwafunga kamba na kisha kuwaweka mahabusu ya kijiji hadi walipotolewa na polisi kutokana na kuwasaliti wananchi na kuwa upande wa mwekezaji.
Mutalemwa Blog ilifika kijiji cha Mihango kata ya kigonsera wilayani mbinga na ilipotamtafuta afisa tarafa tarafa ya Kigonsera Bw.Ilomo na afisa mtendaji wa kata ya Kigonsera Bw.Mngongo iliambiwa kuwa wamepelekwa hospitali kutibiwa baada ya kuondolewa mahabusu ya kijiji.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Bi.Senyi Ngaga amethibitisha kuwepo kwa mgogoro huo na kakanusha kupigwa kwa afisa tarafa Bw.Ilomo na kusema aliyepigwa ni mtendaji wa kata ya Kigonsera na mwananchi mmoja ambapo Bi.Ngaga amesema amemsimamisha mwekezaji hadi maafikiano baina yake na wananchi yatapofikiwa huku mwenyekiti wa kijiji cha Mihango Bw.Damian ndunguru akisikitishwa na kitendo cha kupigwa afisa tarafa ya kigonsera na mtendaji wa kata ya Kigonsera.
Mutalemwa Blog ilipoenda ofisi za kampuni ya AVIV ili wazungumzie sakata hilo wamesema kuwa hadi atakapokuja mkurugenzi mkuu wa kampuni ya AVIV Bw.Meddu Medapa ambaye kwa sasa yu safari ndiye anaweza kulizungumzia.
Post a Comment