Naibu waziri ofisi ya rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi,Suleiman Jafo,amempa wiki tatu mkurugenzi wa manispaa ya ilala,Isaya Mngurumi,kuhakikisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato na uendeshaji wa soko la ilala unabadilika tofauti na sasa ambapo kumekuwepo na upotevu mkubwa wa mapato.
Mh.Jafo ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam,alipotembelea wafanyabiashara wa soko hilo na kusikiliza kero zinazowakabili lakini pia akamwahidi mkurugenzi huyo kuwa atarudi baada ya muda huo akute mfumo wa ukusanyaji wa kodi za kero kwa wafanyabiashara ambazo zinaingia kwenye mifuko ya wanjanja umesharekebishwa.
Baadhi ya wafanyabishara wa soko hilo, wamelalamikia ushuru ambao wamekuwa wakitozwa kunaingia kwenye mifuko ya watu binafsi huku wabeba mizigo nao wakitozwa ushuru ingawa hawana eneo la bishara na mama lishe wakalalamikia kufanya biashara kwenye vizimba ambavyo wanaomiliki wake wanawalipisha 80,000 hadi 100,000 kwa mwezi wakati wao wanailipa halmashauri sh. 9,000 kwa mwezi.
Akijibu sababu za ukusanyaji wa mapato holela katika soko hilo, mkurugenzi wa manispaa hiyo, Mngurumi,amesema wanaoshiriki kukusanya sh.400 ni wafanyabishara wenyewe ambao wamejiunga na vyama vyao vya ushirikia.
Post a Comment