Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

SHULE YA MSINGI ITETE INA DAWATI 1 TU KWA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA, ZAIDI BOFYA HAPA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Katika hali isiyo ya kawaida Wanafunzi 275 wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Itete wilayani Mbozi mkoani Songwe wanalazimika kukaa chini wakati wa masomo kutokana na uhaba wa madawati shuleni hapo.

Kwa mujibu wa Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Mkoloma, darasa la kwanza lenye wanafunzi 278 lina dawati moja pekee lililopelekwa shuleni hapo na mzazi wa mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka mtoto wake akae chini.

Uwepo wa dawati hilo moja unatoa fursa kwa mtoto wa mzazi huyo kuteua rafiki zake wengine wawili kukalia dawati hilo wakati wa masomo hivyo wanafunzi wengine 275 hulazimika kukaa chini.

Mwalimu Mkoloma amebainisha hayo kwenye mkutano wa wazazi na wadau wa elimu shuleni hapo uliofanyika jana ukiwa na lengo la kuelimisha jamii juu ya dhana ya Sera ya Elimu bure pamoja na kujadili changamoto inayoikabili shule hiyo ikiwemo mlundikano wa wanafunzi madarasani pamoja na uhaba wa madawati.

Amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 2000 wa kuanzia darasa la awali hadi la saba na wanafunzi wa darasa la kwanza pekee wapo 278 kati yao ni wanafunzi watatu tu ndio wanaokaa katika dawati moja lililotengenezwa na mmoja wa wazazi wa mtoto ambaye alifika shuleni hapo na kukuta mwanae anakaa chini wakati akisoma.

Mkuu huyo wa shule alisema kwa sasa uhitaji wa madawati shuleni hapo ni madawati 463 kwani kwa sasa shule ina madawati 248 ambayo yamegawanywa katika vyumba vya madarasa 11,hivyo kuiomba serikali na jamii kulitazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi haraka iwezekanavyo ili kunusuru watoto hao kutofanya vibaya kitaaluma.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Mussa Mlele alisema wao kama wazazi wamesikitishwa na hali hiyo hivyo kuwataka wazazi wenzake kuungana pamoja ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo la madawati shuleni hapo badala ya kungoja serikali akisema wanaoumia ni watoto wao wazo lililoungwa mkono na wananchi wenzake.

Chanzo: Jamii Forum


Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top