Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

FAIDA ZA KIAFYA MTU ANAPOKULA MBEGU ZA MABOGA, ZIKO HAPA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Faida za kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi ama zilizokaangwa:


KINGA DHIDI YA MARADHI YA MOYO
Mbegu za Maboga (Pumkin Seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya Magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa ya damu na ufanisi wa utumbo mpana. Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi.

KINGA YA MWILI

Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini aina ya Zinc, ambayo yana faida nyingi mwilini, zikiwemo uimarishaji wa kinga mwilini, ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Vile vile Zinc huimarisha nguvu za kiume.

SARATANI YA KIBOFU

Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha Zinc, utafiti umeonesha kuwa mafuta na mbegu zenyewe za mabogo huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.

KINGA YA KISUKARI

Utafiti umeonesha pia kuwa mbegu za maboga huweza kuimarisha utokaji wa ‘insulin’ mwilini, hivyo kuwa kinga au kuleta ahueni kubwa kwa wagonjwa wa kisukari.

TIBA KWA WALIOFIKIA UKOMO

Mafuta ya mbegu za maboga hayana madhara, zaidi yana kirutubisho muhimu cha kurekebisha Cholesterol mwilini, kushusha shinikizo la damu, kuzuia uvimbe, maumivu ya kichwa, maumivu ya viungo vya mwili na vile vile huondoa maumivu mbalimbali yanayowapata wanawake wenye umri mkubwa waliofikia ukomo wa hedhi (Menopause).

UGONJWA WA INI

Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo, mbegu zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.

USINGIZI

Kwa watu wenye matatizo ya usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kuwa mbegu za maboga zina kirutubisho kinachochea uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi.

UVIMBE

Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, yakiwemo ya kuvimba miguu, vidole na hata majipu.

JINSI YA KULA MBEGU

Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizosafi ambazo hazijakaa muda mrefu. Kwa usalama zaidi, zioshe kwa maji safi kisha zianike, inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini pia ukiamua kula za kukaanga bado utapata faida zake, muhimu usiziunguze wakati wa kukaanga. Kwa kawaida hukaangwa kwa muda usiozidi dakika 10

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top