Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Kile ulichokuwa hukifahamu kwenye ugonjwa wa Sikosell kipo hapa

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Seli Mundu ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika chembe nyekundu za damu, kwa kawaida chembe nyekundu za damu zina umbo la mviringo ambazo huzirahisishia kupita kwenye mifupa midogo ya damu ili kusafirisha hewa safi ya oksijeni katika sehemu mbalimbali za mwili, pia kwa mtu mwenye ugonjwa huo chembe hizo zinakuwa za tofauti na zinanata huku zikiwa na umbo la mwezi mchanga.

Huu ni ugonjwa wa kurithi wa kupungukiwa damu, ambapo mgonjwa huwa hana damu ya kutosha kwa sababu ya seli zake za mwili sio imara kubeba hewa ya oksijeni kupeleka sehemu mbalimbali za mwili, katika nchi tano zinazoongoza kuwa na wagonjwa wengi Tanzania imeshika nafasi ya tano ya kuwa na idadi ya wagonjwa wa siko seli huku ikiongozwa na nchi ya India, ambapo inakadiriwa  asilimia 13 ya watu wote nchini wana visababishi   vya ugonjwa huo, Mratibu wa kitengo cha seli mundu kutoka katika hospitali ya taifa Muhimbili Dk Deogratius Soka anasema Kila mwaka zaidi ya watoto 10,000 nchini huzaliwa wakiwa na matatizo kwenye chembe nyekundu za damu zao na kupelekea kupata ugonjwa wa siko sell au seli mundu.

Pia anasema asilimia 70 ya watoto wanaozaliwa nchini kila mwaka wana uwezekano wakupoteza maisha kama watakuwa hawakupata matibabu stahiki, Soka alieleza kuwa vinasaba vya siko seli hurithiwa kutoka kwa wazazi wote yaani baba na mama hivyo mtoto anaweza akazaliwa na ugonjwa huo ambapo vinasaba vya siko sell hurithiwa sawasawa kutoka kwa wazazi wote wawili.

Huku mmoja wa madaktari katika hospitali hiyo Denisi Kanyika alisema dalili za ugonjwa wa Seli mundu ni pamoja na upungufu wa damu mara kwa mara kutokana na chembe nyekundu za Siko seli hasa watoto hupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo wapo katia hatari ya kupata upungufu wa damu ya mara kwa mara, Maumivu makali, kukwama kwa seli hizi ambazo shepu zake zimekaa vibaya huzuia damu nyingi kupita kwa urahisi  katika mishipa midogo ya damu na kuweza kukwama na kuziba mzunguko wa damu hali hiyo husababisha maumivu makali sana katika viungo vya mwili, maumivu hayo huwa ya jointi, kifua na tumbo mara nyingi.

Kubanwa na kifua, kunasababisha kukwama na kuziba kwa mzunguko wa damu kwenda kwenye mapafu husababisha matatizo katika upumuaji, dalili zake ni kuona maumivu ya kifua, kukohoa, homa na kupumua kwa shida.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top