Maendeleo huletwa na watu, watu wenyewe ndio sisi tukishirikiana na viongozi wetu ndipo tunaweza kupiga hatua chanya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
|
Ikiwa imepita miezi michache ndani ya mwaka huu wa 2017 tayari zimeonekana alama za vijiti zinazo ashiria njia za uwekaji wa nguzo za umeme.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa |
Alama izo zimetokea eneo la Vikindu zimepita eneo la Kazole mjini, Kazole shule ya msingi iliyopo mpakani na eneo la Hamidu na nguzo ya mwisho imeishia Kazole Magenge 20 eneo la njia panda ya kwenda kwa Bakhresa ambapo ndipo mpakani mwa Kazole na Cheta.
Sasa kuanzia hapo mpakani mwa Cheta na Kazole kwenda hadi mpakani mwa Cheta na Magodani hakuna alama yoyote inayo onyesha kuwa nguzo za umeme zitapita ili kwenda mpaka Magodani.
Cheta ipo ndani ya Kazole uku ikipakana na Magodani ila viongozi wa kazole kwa ujumla wamekuwa wakipasahau sana Cheta.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
|
Baada ya uongozi wa Magodani kuchonga barabara yao kuanzia mpakani mwa Cheta kuelekea kwao ndipo Kazole wao walisimika alama za kuonyesha njia za nguzo za umeme zitakapo pita na wao wakaishia mpakani mwa Kazole na Cheta
Je Cheta inayoachwa katikati inaongozwa na akina nani?? Na je kama ina viongozi wake ivi wao wanatambulika upande wa Magodani au upande wa Kazole?? Wananchi wanataka kufahamu.
Kumbuka wakazi wote wa maeneo ya Mwasonga, Magodani, Cheta, Kazole na Vikindu wanategemea Barabara inayoanzia Vikindu hadi uko Mwasonga pamoja na maeneo mengine ambayo sikuyataja sasa je kama maendeleo na miundo mbinu vinawekwa mwanzoni mwa eneo na mwishoni bila kupaunganisha katikati je kunatengeneza kitugani jamani??
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
|
Wananchi wa Cheta wanataka maendelea ya kweli kwa vitendo nasio maendeleo ya kuongea mdomoni na kuwadanganya kwenye mikutano ya vijiji inayofanyika.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara safi, Shule ya msingi na ya Sekondari, Hospital, Soko, Umeme, Visima vya Maji masafi, Viwanja vya Michezo, Sehemu za ibada (Miskiti/Makanisa), Maziko nk.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule ya msingi na ya Sekondari, Hospital, Soko, Umeme, Visima vya Maji masafi, Viwanja vya Michezo, Sehemu za ibada (Miskiti/Makanisa), Maziko nk.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
|
Kwa habari zaidi juu ya wakazi wa Cheta, Kazole na Magodani tazama apo chini.
CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WAKAZI WA KIJIJI CHA KAZOLE NA VITONGOJI VYAKE ZIKO HAPA
[Bofya hapa kusoma]
ILE BARABARA INAYOANZIA VIKINDU GETINI KWENDA HADI MAGODANI NDIO HII
[Bofya hapa kusoma]
KUTOKA PWANI: HIKI NDICHO KIJIJI CHA KAZOLE PAMOJA NA VITONGOJI VYAKE
[Bofya hapa kusoma]
CHANZO CHA KUZOROTA KWA MAENDELEO KWENYE KIJIJI CHA KAZOLE NA VITONGOJI VYAKE IKI HAPA
[Bofya hapa kusoma]
ENEO LA HEKARI 2 LINAUZWA, LIPO KWENYE KIJIJI CHA CHETA
[Bofya hapa kusoma]
ENEO LA HEKARI 17 LINAUZWA / 17 HECTARES FOR SALE, GO HERE NOW
[Bofya hapa kusoma]
Post a Comment