Wazee wa CCM bado
Kufanyika kwa kikao cha Baraza la Ushauri wa Wazee wa CCM kunasubiri uwepo wa wajumbe wake muhimu ambao kwa sasa wako safarini.
Kikao cha wazee hao ndio kitakuwa msingi wa uamuzi wa Kamati Kuu kuwapata wanachama watano ambao majina yao yatapelekwa kupigiwa kura na Halmshauri Kuu na Mkutano Mkuu wa CCM.
Kikao hicho cha Baraza la Usahauri linaloundwa na wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu wa CCM kipo chini ya uenyekiti wa Ali Hassan Mwinyi, ambaye aliongoza Serikali ya Awamu ya Pili, huku katibu wake akiwa Pius Msekwa.
Wengine wanaounda baraza hilo linalotambuliwa na katiba ya CCM ni Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, Rais msataafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu, John Malecela na Amani Abeid Karume ambaye ni Rais mstaafu wa Zanzibar.
Katika mahojiano na gazeti hili jana kuhusu mkutano wao, Msekwa alisema: “Kikao hakijafanyika, wazee wapo safarini. Wengine wapo huko, wengine kule, mimi nipo Dodoma, nitarejea Dar es Salaam baada ya vikao vya Bunge kumalizika.
Alipotakiwa kueleza kama kwa mazingira hayo kikao hicho kitafanyika lini, Msekwa alisema: “Kikao kitafanyika tu, kipo kwenye ratiba. Watu wenye busara husubiri ratiba ikamilike, iko ratiba nasi tunafuata ratiba.”
Post a Comment