Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MKULIMA ANAYEGOMBEA URAIS ATUMIA MABASI YA ABILIA KUTAFUTA WADHAMINI

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Dar/Mikoani. Kada wa CCM, Elidephonce Bilohe (43), mkulima anayeomba kupitishwa na chama chake kuwania urais, amesema anatumia usafiri wa mabasi ya umma kuzunguka mikoani kusaka wadhamini.

Wakati Bilohe akitumia usafiri huo, wagombea wenzake wanatumia au walitumia mabasi waliyokodi na kuyafanyia maboresho ndani, magari madogo na ndege kutafuta wadhamini 450 kutoka mikoa 15 inayotakiwa kwa mujibu wa taratibu za CCM.

Akizungumza na Mwananchi jana, Bilole alisema ameshafika mikoa tisa ambayo ni Dodoma, Kigoma, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Morogoro na Dar es Salaam, tangu alipochukua fomu hiyo Juni 9.

“Huko kote nimekuwa nikienda kwa kutumia usafiri wa mabasi ya abiria na daladala. Kwa kweli nimepata ushirikiano mzuri kutoka kwa makatibu wa CCM, nawashukuru sana,” alisema.

Bilohe alisema atakwenda mikoa 15 tu kama inavyotakiwa na chama chake, tofauti na watiania wengine ambao baadhi wamekwenda zaidi ya mikoa 20. “Kwenda mkoa mmoja natumia siku mbili ama tatu kufika na kupata wadhamini. Gharama ni nyingi sana, lakini kwa kuwa nimeshaamua kuwatumikia Watanzania nitakwenda,”alisema.

Alisema Watanzania wamekuwa wakimtia matumaini katika safari yake hiyo na kuwaomba wamuombee ili aweze kuifanikisha kwa mafanikio. “Naomba Watanzania wenzangu mniombee katika safari hii.

Nitawavusha kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi,” alisema Bilohe aliyejiunga na chama hicho mwaka 2003. Alisema kuwa atazirudisha fomu hizo Juni 30 au Julai Mosi kulingana na ratiba yake ya kukusanya wadhamini.

Jumla ya makada 39 wamejitokeza kuwania nafasi hiyo na Bilohe ndiye mgombea pekee aliye na elimu ndogo ya darasa la saba, tofauti na sheria ya nchi inayotaka mgombea wa nafasi hiyo ya juu kisiasa awe na shahada.

Bilohe ni mmoja wa makada wachache waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM ambao hawajawahi kushika madaraka makubwa serikalini au ya kisiasa.

Katika kinyang’anyiro hicho kuna mawaziri wakuu watatu, mawaziri 12 wa sasa, Jaji Mkuu mstaafu, maofisa wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa, maofisa waandamizi wa Serikali ambao wamestaafu na wabunge.

Mkoani Pwani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amesema kiongozi anayetaka kuwa rais mwaka huu ni lazima alingane kiuadilifu na viongozi wanne wa urais waliotangulia kuiongoza Tanzania kwani hao wote hawakujilimbikizia mali na wanachukia ubadhirifu, rushwa na ufisadi.

Membe alirejea kauli yake kuwa ana sifa zote za kumrithi Rais Jakaya Kikwete na hivyo ameitaka Kamati Kuu kutolikata jina lake ili Tanzania isonge mbele kiuchumi na kiutamaduni.

Membe alipata wadhamini 21,000 na kusema kuwa mkoa huo umevunja rekodi kwa kutoa idadi hiyo ikilinganishwa na mikoa 26 aliyokwishapita.

Waziri huyo alisema akipata urais tu, utakuwa mwisho wa mauaji ya watu wenye ulemevu wa ngozi na kwamba ataanza kumsaka muuaji wa kwanza wa albino na akimkamata tu utakuwa mwisho wa tabia hiyo kwa wengine.

Kadhalika, Membe alisema endapo CCM itampitisha na kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao na kushinda, jambo la kwanza ni kufufua viwanda na kujenga vipya ili kuweza kuzalisha ajira za kutosha.

Alisema atakuwa mkali katika kukataza viongozi kujihusisha katika ulaji rushwa huku akibainisha baadhi ya vipaumbele kuwa ni utawala bora na uchumi wa viwanda.

Akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Morogoro mtaa wa Makongoro mjini hapa mara baada ya kukabidhiwa fomu za wadhamini 950, Membe alisema kuwa Kamati Kuu ya CCM haitakuwa imefanya makosa wala kujuta endapo itamteua kupeperusha bendera ya chama hicho, akiwa na lengo kuu kuzalisha ajira kwa vijana kwa kufufua viwanda vilivyokufa sambamba na kujenga vipya.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top