Leo katika kipindi cha kero yangu, tutaongelea juu ya magari ya abiria ambayo mda mwingi waga radio za magari hayo uwa zinafunguliwa kwa sauti kubwa kiasi kwamba abiria anapotaka kushuka waga inakuwa tabu hasa pale kondakta anapokuwa mbali na abiria halipo, jambo ambalo umlazimu abiria kugonga sehemu moja wapo ya gari husika.
Leo kumetokea kero yanamna hii kwenye gari aina ya Eicher, mali ya Jabir P. Ltd lenye namba za usajiri wa T 650 CLF linalotoa huduma kati ya Mbagala rangi tatu to Kariakoo via Kilwa road.
Kitendo cha dreva kuweka sauti kubwa ya radio kwenye gari hilo abilia walipaza sauti wakimtaka dreva apunguze sauti au kama hawezi basi azime kabisa radio, dreva halikataa kufanya vile abiria walivyokuwa wakitaka na ukizingatia ilikuwa ni asubuhi.
Sasa naomba kuwauliza wanausalama je ni sahihi gari la abiria au gari binafsi kufungulia sauti kubwa wakati gari hilo likiwa linatembea barabarani?? Binafsi naona sio sahihi kabisa.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment