Habari za leo ndugu, leo nakuletea tukio ambalo lilitokea siku ya jana jioni mida ya saa kumi na mbili hivi pale kwenye bus stop station posta nyuma kidogo ya TRA Samora avenue.
Tabia ya abiria kudandia daladala kabla haijasimama sehemu yake imemsababishia majeraha makubwa kijana ambaye sikuweza kufahamu jina lake huku wenzake wawili wakinusurika kwenye tukio hilo la kupata ajali.
Mchezo mzima ulikuwa hivi, daladala ya mbagala ilikuwa ikiingia station bus stop wakati inaingia watu watatu waliidandia gari hilo kabla yakusimama ghafla watu wawili ambao ni baba mtu mzima na mwanafunzi walidondoka huku kijana aliyesalia mguu wake ukanasia chini ya ngazi ya mwisho ya gali na kuanza kuburuzwa chini na gari hilo.
Baada ya abiria waliokuwa kituoni hapo kupiga kelele ndipo dreva alisimamisha gari hilo na kuangalia nini Kilichotokea, ndipo kumkuta kijana yule akiwa amekwanguka nyama kwenye mguu wake pamoja na sehemu ya mkononi kama inavyoonekana hapo pichani.
Kondakta wa gari ambalo kijana huyo alipata ajali hiyo alipewa Tsh 5,000/= kama pesa ya kupatia matibabu ya hawali hospitalini. Katika tukio hilo dreva na kondakta wa gari lililosababisha ajali hiyo hawana makosa hata kidogo maana gari lilikuwa ndo linaingia kituoni kuwashusha abiria kisha kupakia upya.
Naomba bitoe wito kwa raia wote kwamba acheni tabia ya kudandia magari kabla hayajasimama sehemu husika maana yaweza kukusababishia uremavu wa kudumu au kifo.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment