Jinsi ya kumpatia huduma ya kwanza mtu mwenye ugonjwa wa degedege au kifafa kwa lugha ya kiingereza huitwa (Convulsions)
Lengo la kutoa huduma ya kwanza kwa mtu mwenye degedege/kifaa ni kutoa mazingira salama hadi pale kifafa kitakapoma.
Iwapo unashuhudia mtu anakakamaa fanya mambo yafuatayo kumsaidia:
1.Kuwa mtulivu na hakikisha wale wote waliowazunguka wanakuwa watulivu.
2.Usijaribu kumzuia mgonjwa kwa kumkandamiza au kushika mikono na miguu
3.Ondoa vitu vyovyote (vigumu au vyenye ncha kali) vinavyoweza kumdhuru mgonjwa.
4.Fungua nguo au kitu chochote kilichoko kwenye shingo ambacho kinaweza kuathiri upumuaji.
5.Weka kitu laini mfano nguo iliyokunjwa chini ya kichwa cha mgonjwa.
6. Msaidie mgonjwa alale upande.
7.Usimpulizie hewa mdomoni; fanya hivyo iwapo hataweza kupumua baada ya degedege kukoma
8.Baki na mgonjwa hadi degedege litakapokoma lenyewe
9.Onesha upendo wakati anaporudiwa na fahamu
10.Iwapo ataonekana kuchanganyiwa, omba msaada.
endelea kuwa nasi kupitia hapa hapa kwenye Tazama Line tukujuze zaidi. pia habari za afya zingine zinapatikana kwenye Mutalemwa Blog katika ukurasa wa afya bofya hapa kuziona na kuzisoma habari hizi za afya.
Post a Comment