Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

TATIZO LA KUUMWA MIGUU/MIFUPA AU MAGOTI (OSTEOPOROSIS)

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Tatizo hili hujulikana kwa jina la kitaalamu kama Osteoporosis. Ugonjwa huu unatokana na kupunguka kwa protini na madini kwenye mifupa (madini chokaa/calcium). Hali hii hupelekea mifupa kuwa milaini na myepesi ambapo inaweza kuvunjika kirahisi.

Kipindi cha utoto hadi kufikia umri wa miaka 30, ni kipindi ambacho mifupa hujijenga zaidi. Baada ya hapo mifupa huwa ina kawaida ya kupoteza madini zaidi.

Tatizo hili linatokea sana kwa watu wazima, hasa zaidi kwaa wanawake ambao wamefikia kipindi cha kukoma hedhi (menopause), kuanzia miaka 50. Ni kipindi ambacho wanawake hupungukiwa na homoni yenye kazi ya kuilinda na kuikinga mifupa.

Tatizo hili huwapata wanawake zaidi kwa kuwa wana mifupa midogo na myembamba kuliko wanaume. Miaka mitano (5) hadi saba (7) tangu mwanamke kukoma hedhi hupungukiwa na madini chokaa kwa asilimia ishirini (20%), zaidi ya wanaume.

Kuanzia miaka 65 hadi 70 wanawake na wanaume hupoteza madini chokaa kwaasilimia sambamba.

MAMBO YA KUFANYA KUONDOA TATIZO HILI 
1. Mazoezi hasa kipindi ambacho umri umepiga hatua
2. Kwa wale wenye uzito uliozidi, jitahidini kufanya utaratibu wa kupunguza uzito huo

3. Jitahidi kupata madini chokaa (calcium) kwa wingi (maziwa freshi, maziwa mgando, mboga za majani) nk ili kuweza kujitibu.
4. Jitahidi kupata Vitamini D (mayai, maziwa, samaki, mboga za majani, pata jua la asubuhi)

    VIRUTUBISHO VYA KUTUMIA MDA WOTE
Kwa wale ambao tatizo limekuwa kubwa, inawapasa kujitahidi kupata virutubisho ili kuirejeshea mifupa nguvu na uimara, pia kuondokana na maumivu ya mara kwa mara.

Virutubisho vifuatavyo vimewasaidia watu wengi sana wenye tatizo kama hili ulilonalo.
                                                 1. Calcium
                                                 2. Chitosan
                                                 3. Lycopen


KUKOSEKANA KWA UTE KATIKATI YA VIUNGO (JOINTS) - CARTILAGE
Kajiraba fulani ambako hujulikana kwa jina la kitaalamu kama “Cartilage” (Katreji) ambako hupatikana katikati ya mifupa.

Kuna kitu fulani huwa kinapatikana katikati ya mifupa miwili ya goti la mnyama (ng’ombe au mbuzi) huwa wengi wanapenda kukila kwenye baada ya kuchemshwa au kupikwa Kama unaijua hii, basi ndio katileji yenyewe.

Katreji inasaidia kuikinga mifupa isiumie. Vilevile inafanya kazi ya kusaidia kuubeba uzito wakati wa kutembea, kuinama, kunyoosha viungo au kukimbia.

Zaidi ya asilimia 85% ya Katreji ni maji, na jinsi umri unavyosonga mbele, maji hayo huwa yana kawaida ya kupungua. Na asilimia 15% ni protini.

Tatizo hili lipo zaidi kwenye sehemu ya magoti. Endapo Katreji inakuwa ina tatizo, husababisha maumivu makali hasa unapotaka kusimama au kutembea, vile vile maumivu husikika kwenye sehemu za mabegani/ kwenye nyonga.

Pia inaweza kusababisha uvimbe kwenye (goti au kwenye nyonga pamoja na kwenye bega). Mtu ambaye katreji yake ina tatizo aidha imelika au kutokuwepo kabisa, anatakiwa kupatiwa vitu au virutubisho ambavyo vitasaidia kuirekebisha katreji yake au kuijaza katreji hiyo kwa upya kabisa.

Virutubisho vifuatavyo ukivitumia ipasavyo vinaweza kukusaidia kama vilivyo wasaidia watu wengi wenye tatizo hili kama lako.
                                       1. Shark Cartilage
                                       2. Calcium
                                       3. Chitosan

Kuwasiliana na daktari waweza tumia namba zifuatazo:
0715 594 564 au 0756 594 564
Au tembelea website yetu www.1000ufahamu.com
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top