Leo nimeamka nikaiangalia bajeti ya serikali ikabidi nifikirie kidogo kwanza maana kuna vitu vinachekesha sana ila kiukweli vinaumiza mno!
Bajeti ya Tanzania ni Tshs trillion 22.4, na Bajeti ya nchi ya Kenya ni Kshs trillion 47, na Idadi ya watu nchini Tanzania ni 50 millions wakati Kenya ni 38 millions, ukubwa wa eneo la tanzania ni 945,000 km za mraba huku Kenya ikikadiriwa kuwa na 540,000 km.
Je unaweza kukubaliana na maneno ya waziri wa fedha kwamba Tanzania inaweza kuwa nchi ya kipato cha kati 2015/2016?, huo kama sio muujiza ni nini?
Kumbuka Kama deni la taifa ni zaidi ya trilioni 35 na mwaka 2015/2016 litakuwa zaidi ya trillion 41na endapo ccm itaendelea kubaki madarakani kwa miaka 5 tu lazima deni la taifa litafikia Tsh trilioni 65 na kwa miaka kumi mbele litakuwa trillion zaidi ya 100.
Kama PAYE imeshuka kutoka 12% - 11% na ushuru wa bei ya mafuta diesel 50%, petrol 100%, mafuta ya taa 150% je nini lengo na madhumuni ya kufanya vile?
Unajua watu waliosoma mathematics kuna kitu wanaiita msawazo linganifu kwa Lugh'a ya kimombo tunasema (balanced equation), hivi unapoacha kuongeza kodi ya pombe na sigara unataka watanzania tuendelee kulewa ili mtukashifu kama ilivyokuwa kwa wanaume wa Rombo au?
Hamjui kwamba ongezeko la kodi ya mafuta litaathiri sector zote hapa nchini? Na Je shilingi ya Tanzania itaendelea kuporomoka kwa kiasi gani? Pia Je kama 40% ya bajeti ya 2014/2015 haikufikiwa sasa unafikiri kuna maendeleo yatakayofikiwa kwa mwaka 2015/2016?
Mimi sidhani ongezeko hili lililoongezeka kama itafikiwa kama labda itokee miujiza Ikiwa bajeti ya maendeleo (development expenditures) imepungua kutoka trillion 6 mpaka trillion 5 na ile ya matumizi ya kawaida (recurrent expenditures) imeongezeka kutoka trillion 13 mpaka trillion 16 je kwa style hii tutafika kweli?
Post a Comment