Unamkumbuka yule Mbunge
wa Mwibara Kangi Lugola aliyeingia Bungeni na bidhaa za kichina huku
akiilaumu Serikali kushindwa kutumia rasilimali zake na kutegemea bidhaa
za nje?.
Hii nyingine imetokea Zimbabwe na kuzua kizaazaa baada
ya Mbunge wa upinzani Priscilla Misihairabwi kutinga Bungeni akiwa na
nguo za ndani za wanawake huku akisisitiza hatma ya raia wake maskini
kutokuwa na uwezo wa kununua nguo hizo.
Katika kikao chicho cha bunge kilichokuwa kikirushwa live na
Televisheni ya Taifa, mbunge huyo wa Chama cha upinzani cha Movement for
Democratic Change ‘MDC‘ alitoa mfuko wa plastiki uliokuwa na nguo hizo.
Baada ya kutoa akamuuliza Waziri wa Fedha na sera za serikali kuhusiana na uingizwaji wa nguo hizo za mtumba ambazo bei yake ni ndogo na husababisha madhara kwa akina mama.
Akijibu swali hilo Waziri wa Fedha Patrick Chinamasa alimtania Mbunge huyo kutokana na uamuzi wake wa kubeba nguo za ndani za akina mama lakini akasema Wizara yake inachunguza suala hilo.
Kufuatia kitendo hicho Mbunge huyo alitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa chama tawala cha ZANU PF kwa madai ya kutumia matamshi ya kibaguzi.
Uchumi wa Zimbabwe umedorora miaka ya hivi karibuni hali iliyosababisha viwango vya umaskini kuongezeka kutokana na kuwepo idadi kubwa ya watu wasio na ajira.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Post a Comment