Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MWANAMKE MATUNZO WALA SIO NAKUPENDA YA MANENO TUPU

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Hapa jamani inabidi tuambiane ukweli, tena bila kufichana! Kuna baadhi ya wanaume ni wabahili sana, yaani kutoa fedha kwa wapenzi wao wanaona shida sana.Visingizio vya kwamba wao siyo mabuzi ndiyo vimewajaa akilini mwao. Utawasikia wakisema; “Mimi siyo buzi bwana, demu wangu halafu nimlipie? Haiwezekani!

Achana na hizo fikra ndugu yangu. Unatakiwa utoe matunzo kwa mpenzi wako. Siyo lazima mpaka akuambie! Ni jukumu lako kufahamu aina za vipodozi anavyotumia.Mnunulie bila kukuambia, mpelekee, kuwa mbunifu, ukiona nywele zake zinaanza kufumuka, mpe fedha ya saluni, tena ikiwezekana mchagulie mtindo uupendao.

Leo asuke rasta za kimasai, baada ya wiki kadhaa unambadilishia mtindo mwingine. Jiulize kama wewe ndiye mpenzi wake halafu unakataa kumpa matunzo, unataka nani amhudumie? Hivi ulivyokutana naye akiwa mzuri, anapendeza unadhani ni nani aliyekuwa anamhudumia?

Nakuhakikishia ndugu yangu, kama huna utamaduni wa kutoa matunzo kwa mpenzi wako tarajia kukimbiwa! Kwa maneno mengine ni kwamba, kama hutoi matunzo kwa mpenzi wako ni kama umemruhusu awe katika uhusiano na mwanaume mwingine ambaye atatoa matunzo.


Ni wajibu wako kumnunulia mavazi, manukato na hata fedha za matumizi yake binafsi. Tatizo hili huwakumba hata wanandoa, hawataki kuwahudumia wake zao, wakidai kwamba wameshaoa! Usimpompendezesha atapendeza? Na asipovutia unadhani nini kitafuata kama siyo kutafuta mwanaume mwingine nje? Upo tayari kusalitiwa?

Inawezekana unashangaa kwa nini wanawake wanakukimbia kila siku, kumbe kuna sehemu fulani huwa unakosea bila kujua. Hapa ndipo kwenye dawa. Ndiyo sehemu pekee utakayoujua ukweli na kuchukua hatua.

Katika sehemu ya kwanza, wiki iliyopita nilianza kwa kuelezea tabia mbili; moja ikiwa kujiangalia upya tabia zako na pili ni kumpa matunzo mwenzi wako.

Lazima wanaume mfahamu kwamba hata gari linapoharibika huhitajika kupelekwa gereji kwa kufanyiwa ukarabati. Vivyo hivyo hata mwanamke anahitajika kupewa matunzo ili aendelee kuwa bora na anayekuvutia.
Ukweli ni kwamba, wanaume wengi hukwepa kutoa matunzo ya karibu kwa wapenzi wao wakidai wanachunwa! Nani amekudanganya ndugu yangu? Kumtunza mpenzi wako siyo kuchunwa.

Mpendezeshe apendeze, usipofanya hivyo wewe unataka nani akutunzie? Kama una tabia hii badilika haraka, maana wanawake wa sasa wapo makini kuangalia wanaume ambao wanatambua wajibu wao.

Kuna mwingine huwa hatoi fedha mpaka siku atakayolala na mpenzi wake, hiyo ni mbaya zaidi maana hisia za kwamba umemnunua huanzia hapo.

Najaribu kuwaweka sawa na kuwakumbusha kwamba mwanamke anahitaji matunzo na kama ukishindwa kumtunza utakuwa unampa mwanya wa kutafuta mwanaume mwingine. Hapo ndiyo mwanzo wa usaliti.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top