MKAZI
wa kijiji cha Igongwa wilayani Maswa mkoani Simiyu, Majingwa Ndushi
(32) amekamatwa na jeshi la Polisi baada ya kutoroka akikwepa kufikishwa
mahakamani kwa tuhuma ya kumuua baba yake mzazi, Ndushi Majingwa (65)
kwa kumkata na shoka kichwani.
Mbele
ya mahakama hiyo, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa jeshi hilo, Mkaguzi
wa polisi Nassibu Swedy, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, Mei 30
mwaka huu, saa tatu asubuhi kijijini hapo.
Alidai
kuwa, kabla ya kufanya mauaji hayo mshtakiwa huyo alifika nyumbani kwa
baba yake akiwa na shoka mkononi na kumkuta akiwa amekaa kwenye kiti na
kisha kuanza kulumbana kwa maneno na hivyo kushindwa kuelewana, ndipo
alipomshambulia kwa kumkata kwa shoka kichwani na kufa papo hapo.
Swedy
alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Tumain Marwa, kuwa chanzo cha
mauaji hayo ni mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kati ya marehemu na
mwanae huyo.
Alisema
mara baada ya kufanya tukio hilo alitoroka lakini baada ya muda mfupi,
alikamatwa na kisha kufikishwa katika kituo cha polisi cha wilaya ya
Maswa.
Hata
hivyo, mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo,
haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji na hivyo kesi hiyo itatajwa
tena Julai 15, mwaka huu, na mshitakiwa amepelekwa rumande.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment