Serikali imeitaka mamlaka ya bandari Tanzania kuhakikisha inarekebisha mapungufu yote yaliyojitokeza katika mtambo maalum wa kupima mafuta yanayotoka katika meli, huku pia ikionyesha kuridhishwa na namna mtambo huo ulivyoanza kufanya kazi zake siku chache zilizopita.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi saa chache baada ya kutoka Dodoma kwa maagizo maalum, aliwasili katika mtambo huu wa kupima mafuta, ambapo miongoni mwa maelezo aliyoyapata kutoka kwa Meneja muendeshaji wa mtambo huo ni kamera zilizopukutishwa na kimbunga kikali katika eneo hilo na kusababisha eneo hilo kukosa kamera za usalama kwa muda sasa.
Mtambo huu maalum wa kupima mafuta ambao umekwisha kupima meli nne hadi sasa na kujiridhisha na kiwango chake cha upimaji, katibu mkuu huyo amesema utaisadia serikali kupata mapato halisi ya kodi ya mafuta huku pia akitoa maagizo kwa maafisa wa bandari.
Meneja wa bandari licha ya kukiri mkandarasi aliyejenga mtambo huo kukiuka mkataba kwa kuweka vifaa vinavyoathiriwa na maji, amesema watajitahidi kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati maagizo ya katibu huyo mkuu.
Kwa mujibu wa serikali ujenzi wa mtambo huu wa kisasa ni moja ya hatua za kuhakikisha inadhibiti mafuta yaliyokuwa yakipotea na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha, ambapo kwasasa hakutakuwa na utata kuhusu mafuta na kodi inayopaswa kulipwa katika bidhaa hiyo.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment