Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WATAFITI WABAINI AINA 800 ZA MBEGU YA NGANO, ZAIDI BOFYA HAPA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.


Watafiti wa Mbegu nchini wamebaini kuwepo kwa aina 800 ya mbegu za ngano, huku baadhi ya mbegu hizo zikiwa na uwezo wa kustawi hata kwenye maeneo yenye joto kali hadi nyuzi joto 40, na kufanya zao hilo liweze kustawi hata maeneo yanayolimwa zao la mpunga, jambo ambalo inaweza kuwa suluhisho la kukabiliana na pengo kubwa la asilimia 90 za mahitaji ya ngano hapa nchini kwa mwaka.

Mtafiti wa Taifa wa mbegu ambaye pia ni mratibu wa mradi wa utafiti na uendelezaji wa zao la ngano wa Sard nchini daktari Rose Mongi, amebainisha hayo mkoani Rukwa wakati alipokuwa akiwatembeza wataalamu wa mradi huo wa Sard kutoka makao makuu nchini Tunisia, 

kuangalia mashamba ya ngano yanayolimwa na baadhi ya wakulima mkoani humo, na kusema kuwa kufuatia nchi hii kuwa na maeneo mazuri ya kilimo, haoni kwanini iendelee kuzalisha tani laki moja tu wakati mahitaji ya ngano nchini ni zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka.

Baadhi ya wakulima wa zao la ngano mkoani Rukwa, wameueleza msafara huo wa aina yake kuwa licha ya kupata mafanikio makubwa baada ya kuanza kutekeleza kilimo cha zao hilo kisasa zaidi baada ya kuachana na kilimo cha mazoea, lakini wanakabiliawa na changamoto za kukosa baadhi ya zana ikiwa ni pamoja na mtambo wa kuvunia ngano.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top