Kesi ya kupinga uamuzi wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu iliyofunguliwa na na jukwaa la asasi za kiraia za Afrika Masharaki imeanza kusikilizwa leo katika mahakama ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana muda mfupi kabla ya uchaguzi wa nchi ya Burundi kufanyika,mshtakiwa wa kwanza ni mwanasheria mkuu wa Burundi, anayelalamikiwa kwa kutoweza kuzuia uamuzi wa mahakama ya katiba ya nchi hiyo kumruhusu Mh.Rais Pierre Nkurunziza kuwania mhula wa tatu.
Mshatakiwa wa pili ni tume ya uchaguzi ya burundi inayolalamikiwa kwa kumkubalia rais Nkurunziza kuwania nafasi hiyo, na mshatakiwa wa tatu ni aliyekuwa katibu mkuu jumuiya ya afrika mashariki anayelalamikiwa kushindwa kutumia kanuni za utawala wa sheria kama zilivoidhinishwa kwenye mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya ya afrika mashariki zisivunjwe na Serikali ya Burundi.
Wakiwa katika Mahakama hiyo mawakili wa pande zote wamewasilisha hoja zao mbele ya majaji wa mahakama hiyo Facky Jundu, Lenaola Issack na Monica Mgenye Wakili wa Serikali ya Burundi Nestory Kayobera ambaye anasema katiba ya Burundi inampa fursa Rais Nkurunzinza kugombea muhula wa tatu na pia Mahakama ya Afrika Mashariki haina uwezo wa kubatilisha maamuzi ya Mahakama ya Burundi.
Naye wakili wa upande wa walalamikaji Donald Deya ambaye anasema kwa mujibu wa Sheria za mkataba wa uliounda jumuiya,Mahakama hiyo inao uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kwamba tayari imeshatolea maamuzi baadhi ya Mashauri.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment