Mjadala wa bunge kuhusu bajeti umezidi kupamba moto baaada ya wabunge wa Chama Cha Mapindunzi CCM kutumia muda huo kuwasema wale wa upinzani na kulaani kitendo cha wao kutoka nje ukumbi hatua ambayo inasababisha washindwe kuonyesha ushiriki wao katika bajeti hiyo ambayo ni dira muhimu kwa taifa kwa mwaka 2016/2017.
Wakitumia dakika tano tano kwa kila mmoja wabunge hao akiwemo Mh Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera wamesema kitendo cha wenzao wa upinzani kususia mjadala huo hakileti afya kwa wananchi wa majimbo wanayoyawakilisha na hivyo watizame upya maamuzi yao
Ushauari huo unakataliwa na Mh Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya mjini ambaye anasema wao wanaamini kuwa kuwawakilisha wananchi siyo lazima kuingia bungeni na ndio maana hata sasa wanafanya vikao vyao vya kuijadili bajeti hiyo katika ukumbi wa zamani wa msekwa na watatumia mbinu zao wanazozijuwa kuwafikishia wananchi wao taarifa za bajeti hiyo.
Hata hivyo kutokana na mvutano huo naibu spika Dk Tulia Ackson analitolea ufafanuzi suala hilo ambapo anasema wabunge wa upinzani kutoka nje wanafanya hivyo kwa utashi wao.
Katika hatua nyingine wakichangia hotuba hiyo Mh Ahmed Shabiby mbunge wa Gairo amesema kwa sasa hali ya fedha mtaani ni ngumu sana hivyo mpango wa serikali wa kuelekeza fedha zote hazina utazidi kuongeza machungu huku Mh Oran Njeza mbunge wa Mbeya vijijini akitaka ofisi ya CAG kuja na mkakati mpya wa kudhibiti fedha za umma.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment