Maendeleo hayana chana wala dini, karibu ndugu msomaji wetu.
Barabara hii ina wastani wa 10km kwa makadirio, barabara hii inaanzia eneo la Vikindu Getini wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, inapitia kijiji cha Kazole kisha kitongoji cha Cheta na kuendelea hadi kijiji cha Magodani na kuunganisha maeneo mengineyo huko mbele.
Apa ndipo vikindu getini ambapo barabara hii uanzia.
Nauri yake kwenda/kurudi ni Tsh 1,000 kwa mtu mzima na Tsh 500 kwa mwanafunzi.
Kwa sasa wakazi wa Kazole, Cheta pamoja na Magodani usafiri wao mkubwa ni magari aina ya Noah ambazo upaki Vikindu, japo kuna daradara tatu zinazotoa huduma kuanzia Mbagala rangi tatu hadi Kazole Magenge 20 nazo hutoza nauri ile ile, ila ikifika kipindi cha masika tu basi magari hayo yote hayatoi huduma tena.
Lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba miundombinu yake ni mibovu kupitiliza, barabara hii kuchongwa yote kuanzia Vikindu hadi Magodani na kuwekwa kifusi pamoja na kurekebisha mitaro pamoja na madaraja yake yote imekuwa kitendawili.
Mwaka 2016 katikati kulitengenezwa madaraja mawili madogo ambayo yapo hadi sasa, daraja la kwanza lipo Mkokozi wa kwanza na lapili lipo Mkokozi wa pili, maeneo haya ni mikondo ya Maji, majibu yake tunayasubili kwenye kipindi cha masika kinachokuja maana ni wazi kabisa kwamba madaraja hayo hayawezi kumudu mshindo wa maji katika maeneo hayo.
Barabara hii ni yamuhimu sana maana ndio barabara pekee inayotumiwa na watu wengi kutoka maeneo mbali mbali.
Changamoto ni nyingi wanazokumbana nazo wakazi wa maeneo tajwa, mpaka sasa hawajafikiwa na umeme, maeneo yao hayaja pimwa, hawana maji safi, hospital, shule za secondary, sehemu za ibada, masoko, maeneo ya michezo, maziko, nk. Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment