Habari za hivi punde nikwamba duka la Palace Mobile Centre lililopo Posta mpya jijini dar es salaam karibu na jengo la Haidary plaza limevamiwa na wezi usiku wa kuamkia leo.
Katika tukio hilo wezi wamevunja makofuri yote na kuingia ndani ya duka hilo na kuchukua simu zote pamoja na sanduku la pesa huku wakiacha makava ya simu pamoja na vitu vidogovidogo tu kwenye display dukani hapo.
Police wamefika kwenye eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa kuweza kubaini chanzo cha tukio hilo, Endelea kuwa nasi ili tukujuze zaidi juu ya tukio hili la wezi kuvamia palace.
Napenda kutoa pole sana kwa mmiriki pamoja na wafanya kazi wote juu tukio hilo na Mungu atawasaidia kuweza kuwabaini wezi waliohusika katika tukio hilo.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment