Zaidi ya wakazi elfu hamsini (50,000) wilayani Arumeru wapo hatarini kupatwa na balaa la njaa.
Bwana Abdi Msuya ambaye yeye ni mwenyekitu wa mfereji wa kipilipili amesema wanakumbwa na janga la njaa wilayani hapo kutokana na utumiaji mbaya wa maji yatokanayo na mfereji wa kipilipili, ambapo matumizi yamekuwa mengi mno kuliko kawaida ambapo kila sekta inategemea mfereji huko kufanya kazi yake ambapo amezitaja baadhi ya sekta hizo nipamoja na sekta ya Kilimo, sekta ya mifugo nk.
Bwana Elishiria Kanuya ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Kwaugoro amesema wameanza kukusanya michango kutoka kwa wananchi kwa ajiri ya kupata pesa za kurekebisha mfereji huo na kuuweka katika hali ya usafi na usalama uku akisema wamefikia asilimia60 za ukusaji wa michango hiyo wilayani hapo.
Katika hatua hiyo ya uchangishaji wa pesa za ujenzi wa mfereji huo mbunge wa Arumeru mashariki Mh. Joshua Nasari alitoa mifuko 300 ya cement kwa ajiri ya kuchangia ujenzi wa mfereji huo wa kipilipili uku lengo likiwa ni kupata mifuko 800 ya cement kwenye kazi hiyo.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment