Habari za leo ndugu wadau wa Tazama Line, leo katika kipindi cha Kero Yangu nimejitosa barabarani na kuibuka na ishu nzima juu ya traffic maeneo ya Kizuiani mbagala jijini Dar es salaam.
Nitaweka mambo wazi na atakaye kerwa basi kimpangowake maana waswahili wanasema hasiekuheshimu nawe usimuheshimu, chanzo cha habari hii ni gari lenye namba T374 BDB
Ndugu zangu mnamo tarehe 23rd May 2015 siku ya juma mosi ya wiki iliyopita nilikwenda kutembea maeneo ya Mbagala rangi tatu nikiwa kwenye gari lenye namba tajwa hapo juu baada yakufika huko mambo yalikuwa hivi:
Tulipofika eneo la Kizuiani tulikutana na traffic wakikagua magari ya abilia na yale ya mizigo, baada ya kulisimamisha gari ambalo nilikuwa nimepanda traffic wawili walikuja mbele ya gari lile kisha wakagawanyika, mmoja akalizunguka gari hilo na mwingine akabaki anaongea na dreva upande wa drisha.
Mala ghafra kondakta wa gari hilo akatenga pesa kiasi cha Tsh 3,000 kisha akatoka nje ya gari lake na akazunguka nyuma ya gari hilo ambapo traffic wa kwanza alikuwa amesimama, baada ya kufika pale yule traffic wa pili aliyekuwa akiongea na dreva naye akaja nyuma ya gari hilo akipitia upande wa pili wa dreva, traffic wote wakawa wako nyuma ya gari
Mazingira ya kupokea pesa kutoka kwa kondakta yakaanza kutengenezwa, yule traffic aliyekuwa akiongea na dreva alikuwa ameshika kitabu cha kutolea recept, na mwingine akiwa mikono mitupu.
Kondakta akatoa ile Tsh 3,000 na kuwapa wale traffic, huku yule traffic mwenye kitabu akawa amewapa mgongo kati ya kondakta na traffic wa pili, wakati yule traffic mwenye kitabu akionesha kidole kwa traffic mwenzake ndipo kondakta alipoelewa mchezo na kumpa yule traffic ile pesa kisha yule traffic mwenye kitabu akarudi kwa dreva akaongeanae kisha dreva akacheka huku kondakta akawa ameisharudi kwenye gari kisha tukaendelea na safari yetu.
Ikumbukwe kwamba gari hilo mbali ya kugundulika lina tatizo lakini halikuweza kutozwa faini kwa kufuata taratibu za kawaida, ambapo dreva na kondakta walitakiwa kutozwa faini kisha kuandikiwa recept inayoonyesha malipo lali, matokeo yake traffic hao walivura Tsh 3,000 yao kisha wakamruhusu dreva aendelee na safari zake.
Je traffic hao wamefanya hivyo kwa magari mangapi kwa siku ya leo? Na je huo ndio utaratibu ulipangwa na mamraka husika?
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment