Ni
nchi iliyoendelea sana Afrika kwa kuwa na miundombinu mizuri kama
barabara na hata majengo ambayo yanaweza kutumika kwa matukio kama haya
ya MTV Mama Awards ambapo event ilifanyika kwenye ukumbi wa ICC Durban South Africa.
Ni
ukumbi ambao June 2015 uliendeleza headlines zake kwa kupigiwa kura
kwenye tuzo ya kuwa ukumbi bora wa mikutano Afrika kwa mara ya kumi na
nne mfululizo kutokana na ubora wake, ujenzi wa kisasa na hata urahisi
wa kupata huduma muhimu unapokuwa ndani yake.
Inawezekana
sababu mojawapo ya utolewaji wa tuzo kubwa za burudani Afrika
kufululiza kufanyika Afrika Kusini ni kutokana na urahisi wa sehemu ya
kufanyikia yani majengo sahihi kwa ajili ya events kubwa kama hizi
ambapo MTV Mama Awards 2015 zilitolewa hapa July 18.
Kwa mara nyingine tena tuzo za MTV Africa 2015
zilifanyika ndani ya hili jengo ambapo Tanzania ilikua ikiwakilishwa na
wawili ambao ni Diamond Platnumz aliyeshinda tuzo ya BEST LIVE pamoja
na Vanessa Mdee.
Post a Comment