1.OSHA UKE WAKO KWA MAJI SAFI KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA HAJA NDOGO.
Asilimia kubwa ya wanawake hawana mazoea na utaratibu huu.Ni utaratibu muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanamke,unapokuwa unajisaidia haja ndogo lazima utakuwa umechuchumaa.
Haja ndogo yako imapokuwa inatoka lazima kutakuwa na mabaki kidogo yatarukia na kubakia lips za nje au za ndani za uke wako.Hayo mabaki baada ya muda yatachanganyika na jasho ma kutengeneza harufu mbaya hivyo ni vizuri kuosha uke wako kwa maji safi kila unapomaliza kujisaidia haja ndogo.
2.UKIWA UNAOSHA UKE WAKO,TUMIA MTINDO WA KUPELEKA MKONO KUTOKA MBELE KURUDI NYUMA.
Kuna baadhi ya wanawake tayari wameshazoea kusafisha sehemu zao za siri kwa kupeleka mkono kutoka nyuma kuja mbele.
Hui mtindo sio mzuri kiafya kwa kuwa huko nyuma kuna sehemu ya haja kubwa, kumejaa uchafu na bacteria wengi, sasa wakati unajisafisha unapopeleka mkono nyuma unazoa uchafu na ukauleta mkono mbele unaacha hao bacteria na uchafu kwenye uke wako.Na huo ndio mwanzo wa uke wako kutoa harufu mbaya na kupata infections za ajabu ajabu.
Ukitaka kuwa salama, haijalishi kuwa umemaliza kujisaidia haja kubwa,au ndogo au wakati unaoga, ukitaka kusafisha sehemu zako za siri, tumia mtindo wa kupeleka mkono mbele kurudi nyums ili usije kuwaleta bacteria na uchafu wa nyuma, mbele kwenye uke wako.
3.VAA NGUO ZA NDANI ZENYE ASILI YA PAMBA.
Pamba ina uwezo wa kupitisha hewa hata kama ni kidogo sana, na sehemu za siri za mwanamke inahitaji flow ya hewa inayopita, nyingine iwe inaingia na nyingine iwe inatoka.
Hii flow ya hewa hata kama ni ndogo itasaidia kufanya sehemu zako zs siri kuwa fresh muda wote na utapunguza uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.Na pia punguza kuvaa nguo za kubana sana muda wote, nguo za kubana zinasababisha majasho sehemu za siri na ukizingatia hamna flow ya hewa kwenye sehemu zako za siri basi lazima hayo majasho yataanza kutoa harufu mbaya.
4.USIVAE NGUO YA NDANI MOJA SIKU NZIMA.
Kwa jinsi maumbile ya mwanamke yalivyo, umatakiwa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku.Unapotoka nyumbani kuelekea kazini, chuo, kwenye biashara zakp n.k hakikisha unatoka na nguo ya ndani ya pili ambayo unatakiwa uiweke ndani ya mkoba au kipima joto chako.
Labda ulivaa nguo ya ndani asubuhi ulipokuwa unatoka nyumbani,ikifika ( saa 8 au 9 ) ingia bafuni au chooni,vua nguo yako ya ndani,kisha unaweza ukaoga mwili mzima au ukasafisha sehemu zako za siri tu.
Ukimaliza hapo chukua nguo ya ndani safi uliyotoka nayo nyumbani uivae,hapo sasa unaweza kuendelea na shughuli zako kama kawaida huku uke wako ukiwa msafi bila harufu za ajabu ajabu.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment