Ikiwa ni siku chache baada ya tukio la uvamizi katika kituo cha
Stakishari,Dar es salaam kutokea, bado matukio ya kutumia silaha
yameendelea kutokea katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
HekaHeka ya leo ni kuhusu tukio lililotokea maeneo ya Mbezi (Mpigi Majohe)…ambapo mama mmoja na mtoto wake wamepigwa risasi na mama huyo kufariki duniani huku mwanaye akijeruhiwa vibaya mgongoni.
Akisimulia tukio hilo mtoto huyo ambaye alikua akiendesha gari huku
mama yake akiwa pembeni anasema alipigiwa na mama yake simu akachukue
mbuzi Vingunguti na kumtaka ampitie Mbezi madukani ili waende wote nyumbani.
Anasema baada ya kumchukua mama yake wakati wanaelekea nyumbani gafla
ilikuja pikipiki ikiwa na watu wawili kisha kuwasimamisha na kumtaka
mama yake atoe pochi yake… lakini licha ya kuwapa walimpiga risasi mbili
moja mguuni na nyingine tumboni na kupelekea kifo chake na yeye kupigwa
risasi ya mgongoni.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment