Mapenzi yanapoangaliwa kila upande, unakuja kupata jibu kwamba hakuna uhusiano uliokamilika. Muhimu kwako ni kumkubali mwenzi wako kama alivyo na kumpa heshima yake ya asimilia mia moja.
Kumkubali ni kutambua ujazo wake moyoni mwako. Hapa nikiwa na maana kwamba wewe mwenyewe unakuwa umejiridhisha kuwa unampenda kwa alama zote, hivyo umeamua kufanya naye maisha.
Uvumilivu unahitajika kwa kila mmoja, lakini busara iliyo wazi ni kwamba hutakiwi kuishi kwa kutazama makosa ya mwenzi wako. Mwisho wa siku naye ni binadamu, kwahiyo unaishi na kiumbe chenye damu na moyo, siyo malaika.
Unashauriwa kumtambua mwenzi wako kwa jinsi alivyo na kujua jinsi ya kurekebisha kasoro zake. Kosoa kwa vipimo, siyo kwa sababu Mungu amekujalia mdomo na sauti ndiyo kila siku upayuke.
“Umeona sasa, mimi nilishakwambia… halafu wewe basi tu, ipo siku yako. Mtu gani hueleweki?” Anayetaka maeno ya namna hii, siku zote hajui kwamba yeye ni binadamu, naye kwa maana moja au nyingine anakosea ila anavumiliwa.
Kosa kubwa kwa wapenzi ni kutaka kuwafanyia mabadiliko wenzi wao. Mmekubaliana leo kuwa wapenzi inamaana kila mmoja kavutiwa na mwenzake lakini siku hazijapita nyingi, masharti yanakuwa kibao.
“Si nilikwambia usiwe unavaa kimini? Halafu huo wanja wako kama paka mapepe!” Taratibu ndugu. Aliyesema Roma haikujengwa siku moja hakukosea, aliona mbali, kwahiyo kumfanya mpenzi wako awe katika kiwango unachotaka, hebu mueleze taratibu kwa lugha inayopenya halafu uvute subira.
Pamoja na maelezo hayo ya upande wa kwanza, mkono wa pili kuna elimu kuwa ni kweli haitakiwi mtu uishi kwa kuangalia makosa ya mwenzi wako, umetetewa usiangaliwe lakini ni lazima uishi kwa hisia za mwenzi wako.
Hapa ndipo ninapogusa nidhamu ya kweli kwenye mapenzi. Ufafanuzi wake unakuwa kwamba unatakiwa kuishi kwa kumuangalia mwenzi wako kama kioo. Wengine wanasema ulinzi unaoipa mboni yako, uwe sawa na ule unaopaswa kutoa kwa mwenzi wako.
Inawezekana uzito ukawa tofauti, nikiwa na maana kuwa nafsi ya kwanza ni yako lakini mantiki ipo. Na ikizingatiwa ujenzi wake ni mkubwa mno kwa sababu hakuna linaloweza kumpendeza mtu anapobaini kwamba mpenzi wake anamjali kuliko chochote.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment