Mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa ameituhumu CCM kuwa
ni hodari wa kuiba kura hivyo akawataka wananchi wajitokeze kwa wingi
kupiga kura ili hata sehemu ya kura hizo ikiibiwa, Ukawa ishinde kwa
kishindo.
Lowassa ambaye ni waziri mkuu wa zamani aliuambia umati wa wafuasi wa
Ukawa uliojitokeza jana kumpokea katika ofisi za makao makuu ya CUF
yaliyopo Buguruni kuwa ili kufanikisha ushindi wa kuwawezesha kuingia
ikulu hawana budi kushikamana, kushawishiana kupiga kura kwa wingi na
kuzilinda Oktoba 25.
Kauli hiyo ya Lowassa ambaye amelelewa kisiasa na CCM tangu
alipojiunga akiwa mdogo mwaka 1977, inaendeleza tuhuma ambazo hutolewa
na vyama vya upinzani kuwa chama hicho huchakachua matokeo wakati wa
uchaguzi.
Hata hivyo, Lowassa hakuwa na vielelezo wala kuthibitisha kuhusu tuhuma hizo dhidi ya chama chake cha zamani.
“Tukiwa na umoja, tukiwa na
mshikamano tutawaondoa Jumapili asubuhi sana. Tutahitaji mshikamano,
tatahitaji ushawishi wa kupiga kura tupate angalau asilimia 90 ili
wakiiba asilimia 10 tuwasamehe,” alisema Lowassa katika hotuba yake
iliyokuwa inakatishwa na kushangiliwa na na salamu ya CUF ya “Hakiii” na
kujibiwa “kwa wote.”
“Hodari sana wa kuiba CCM kura. Sasa tupate kura nyingi za kutosha hata wakiiba kura hausikii na kuna usemi wa Chadema unaosema ‘piga kura, linda kura’ na sisi CUF ni hodari sana wa mambo hayo.”
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipotafutwa kwa simu
kuhusu madai hayo, alijibu kwa ujumbe wa maneno kuwa asingeweza
kuzungumza bali atumiwe ujumbe, na alipotumiwa ujumbe huo hakujibu.
Akizungumzia madai hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu, Damian Lubuva alisema Lowassa angeeleza jinsi wanavyoiba kura.
“Ili kutoa majibu ya uhakika
naomba tufanye utafiti wa kutosha juu ya tuhuma hizo, lazima tujue ni
njia zipi watu wanaiba, vinginevyo nitaeleza kitu ambacho sina ufahamu
nacho. Yeye (Lowassa) kama mtu aliyekuwa serikalini lazima ana ufahamu
walikuwa wanaiba vipi, angeeleza.”
Tume huwa inaendesha uchaguzi kwa mujibu wa taratibu na sheria na
iwapo kuna mtu anasema kura zinaibwa ajitokeze aeleze kinagaubaga ili
ofisi yake ifanye utafiti wa kina.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment