Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata
wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani hapo,
alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi
ni wapumbavu na malofa.
“Kuna vyama vinajifanya
vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na Tanu, hao
wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii
ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuiomboa kwa kupambana ana
umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali
zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja
itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.
Alisema kati ya wagombea urais wanane waliopitishwa na Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (Nec), hakuna mwingine mwenye sifa nzuri kama Dk. Magufuli.
Katika hatua nyingine, alisema haitoshi kuchukia umaskini bali
inatakiwa mtu aeleze ni namna gani ataweza kupambana na tatizo hilo.
“Eleza ni kwa namna gani utapambana na umasikini, ilani ya CCM inaonyesha namna ya kutekeleza kama alivyofanya Dk. Kikwete,”Mkapa.
Aliwataka wanachama wa CCM kuwashawishi Watanzania kuipigia kura CCM
ili kuendeleza ukombozi wa maendeleo ya Tanzania na ushindi ni lazima
kwa CCM.
Kwa upande wake Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, naye aliwarushia vijembe wapinzani kwa kusema kuwa ni CCM B na kwamba hakuna sababu ya kuwachagua kwa sababu CCM A ipo.
“Wanaohama wenyewe wamesema kwa
nini wanaenda huko, siyo mimi ninasema, wanasema wanaenda kuwafundisha
namna ya kuioandoa CCM, kwa hiyo dhamira inayowapeleka huko ni kutafuta
namna ya kuishinda CCM hali iliyosababisha kutengeneza CCM mbili ambazo
ni A ya kwetu na B ni ile ya upinzani mliyoisikia wenyewe, kama A ipo B
ya kazi gani?,” Mwinyi.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, alisema sababu za ufisadi ni viongozi kuwa karibu na matajiri.
“Miaka 20 iliyopita Mkapa alinipakazi ya kuangalia ufisadi,
katika taarifa ile tulisema chanzo cha ufisadi ni viongozi kuwa jirani
na matajiri, ‘mmewahi kumwona Magufuli yupo karibu na matajiri?
“hapanaa”, wananchi walijibu.
Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
alisema Magufuli ni mzalendo hasa kwa nchi yake akiwa pamoja na mgombea
mwenza wake, Samia Suluhu Hassan.
Alisema pia kwamba, Dk. Magufuli amechaguliwa na chama chake
kumetokana na mgombea huyo kuwa na sifa za uadilifu, uchapakazi na
uzalendo.
Kwa upande wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohammed Shein, alisema Wazanzibari wapo pamoja na Dk. Magufuli kama ambavyo waliwaunga marais wengine waliopita.
Hata hivyo Dk. Sheni alisema ushindi wa CCM uko wazi huku akijigamba
kuwa vyama vya upinzani haviwezi kufurukuta kwa upande wa Zanzibar.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment