Watu wa makundi kadhaa wametoa kauli tofauti kuhusiana na hatua ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na upinzani.
Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Danford Kitwana,
alisema kuhama kwa viongozi waandamizi wa serikali na makada maarufu wa
chama tawala, ni ishara ya mwelekeo mbaya kwa chama hicho kwani hadi
Oktoba idadi kubwa wanahamia inaweza kuongezeka.
“Ni ishara ya mwelekeo mbaya
kwa CCM, maana ndiyo kufunuliwa kwa siri za ndani za CCM ambazo upinzani
wanazihitaji…..kunaongeza uwiano mzuri baina ya upinzani na CCM,” alisema.
Mkazi wa Dar es Salaam, Joseph Masaga, alisema hiyo ni ishara kwa
chama tawala kuwa katika hatari ya kupoteza nguvu kutokana na malalamiko
ya wananchi dhidi ya mfumo wa kupata viongozi wake.
Aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba cha KCMC, Prof. Watoki Nkya,
alisema hatua ya Sumaye inaashiria kwamba umri wa kuishi wa CCM hicho
umefikia ukingoni, kutokana na kukua kwa demokrasia nchini.
Mhadhiri Msaidizi wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Iringa (UoI), Emanuel Damalo, alisema uamuzi huo unaweza kuwa ni ishara mbaya ya kuanguka kwa CCM, baada ya kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50.
Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (RUCo), Rwezaura Kaijage, alisema: ”Mimi
nawashauri CCM badala ya kuwakejeli na kuwasimanga wanaohama, wangekaa
chini wakatafakari nini kinatokea, huu upepo siyo mzuri kwa watawala.
Alisema haua ya kuhama kwa Sumaye na Lowassa (Edward) si ya kabeza, lazima ujiulize kuna nini ndani ya CCM.
Mwanasheria wa mjini Morogoro, Deo Niragira, alisema
ni uamuzi wa busara kutokana na kutotendewa haki alipokata rufaa baada
ya kupewa adhabu ya kifungo cha miezi 12 kwa madai ya kuanza kampeni za
kuteuliwa kuwania urais kabla ya muda wake.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk. Joel Mmasa, alisema
Sumaye ni mmoja wa viongozi wachapakazi ambaye alimsaidia kwa karibu
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye mpaka sasa amebaki na kuwa
na sifa kukuza uchumi, hivyo hatua yake inaweza kuiathiri CCM uchaguzi
wa Oktoba.
Mwenyekiti wa Chama cha Biashara (TCCIA), Mkoa wa Mbeya, Dk. Luitico Mwakalukwa, alisema alichokifanya Sumaye ni jambo zuri kwa kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha upinzani.
Mwenyekiti wa Mtandao wa wasomi Mkoa wa Mbeya, Prince Mwaihojo,
alisema baada ya kukaa kwa muda mrefu ndani ya CCM tangu alipostaafu,
Sumaye ameona hasikiki na sasa anatafuta mahali ambako anaweza
kusikika.
“CCM hawapaswi kupuuza suala
hili kama kweli ni chama kinachojitambua na walipaswa kulifanyia kazi
tangu alipoondoka Lowassa, lakini kuishia kupiga vijembe tu huku
wanachama wakizidi kuwakimbia haisaidiii, bali wanajimaliza kisiasa,” alisema Sembuyagi Omary, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria (OUT), jijini Tanga.
Dk. Lupa Ramadhani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
alisema ni jambo la kushtua katika siasa za nchi hii na linaonekana la
kushangaza pale viongozi wakuu ambao waliwahi kushika nyadhifa kubwa
ndani ya serikali kukihama chama tawala.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment