Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetumia zaidi ya Sh. bilioni 218
kwa uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa
mfumo wa kielektroniki wa Biometric Votes Registration (BVR) pamoja na ununuzi wa mashine na vifaa vya BVR kits.
Mkurugenzi wa Nec, Kailima Ramadhani, alisema Sh. bilioni 133 zilitumika kununua mashine za BVR 8,000 zilizotumika kuandikisha wapiga kura.
Alisema Sh. bilioni 85 zilitumika katika uandikishaji kikiwamo kulipa
posho waandikishaji, opereta, kutengeneza kadi, karatasi, wino na vifaa
muhimu vilivyohitajika kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo 99.5.
Alisema, lengo lilikuwa kuandikisha wapigakura 23, 913,184 na hadi
uandikishaji unakamilika Agosti Jumanne iliyopita, wapigakura 23,782,558
wameandikishwa. Kailima alisema maandalizi ya msingi yamekamilika, ikiwamo kuwapata
wazabuni wa kusambaza vifaa hivyo ambao watajulikana baada ya Agosti 21,
mwaka huu.
“Maandalizi yote yamekamilika,
hatuwezi kuchapisha karatasi kwa sasa tunasubiri taarifa za wagombea
wakaopitishwa kutoma kwenye vyama vya siasa, kwa maana ya chama, jina,
picha, eneo na nafasi anayogombea…tunaweza kuweka majina halafu
wakiwekewa pingamizi tutatakiwa kuchapisha tena,” alisema.
Kuhusu malalamiko yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu mwaka 2010,
Kailima alisema hakuna ukweli wowote wa kuhama kwa tiki iliyowekwa na
mpigakura kwenda kwa mgombea ambaye hakumchagua.
Alisema kuna kamati mbalimbali zenye wajumbe kutoka ndani ya vyama
ambao hushiriki hatua zote na kwamba hakuna atayekubali kuona chama
chake kinahujumiwa. Aidha, alirejelea kauli ya Nec kuwa watu watapiga kura katika maeneo
waliyojiandikishia na ambao watapigia maeneo mengine watakuwa na fursa
ya kuchagua Rais pekee.
Post a Comment